HABARI KUU:

GACHAGUA ALIYEMUITA RAILA MAJINA SASA AMMEZEA MATE 2027..//..LUSAKA AMKAUKIA SENETA ONYONKA KWA KUMUITA MPUMBAVU!..//..GEN Z WA BANGALADESH WAVAMIA IKULU YA WAZIRI MKUU..//..AJALI SACHANGWAN HUKU WANAFUNZI 25 NA WAALIMU 3 WAKIPATA MAJERAHA MABAYA..//..MGOMBEA urais wa Chama cha Democrat Kamala Harris amemteua Gavana wa Minnesota Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa urais wa Novemba 5, mwaka huu.// AMERIKA imeonya serikali ya Kenya Kwanza dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi kukabili waandamanaji na kutaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu..//GAVANA wa Meru Kawira Mwangaza anataka Mahakama Kuu kuwahukumu maafisa wawili wa bunge la kaunti na MCA aliyeteuliwa kwa madai walidharau mahakama, akisema walipuuza maagizo ya korti kwa kukusudia kumtimua kwa mara ya tano.

Monday, 16 September 2024

WANAFUNZI WA ZAMANI WA MANORHOUSE WAOMBOLEZA KIFO CHA BABA WA MWENZAO

 


Wingu la majonzi ligubika jamii ya zamani ya shule ya upili ya manorhouse baada ya mmoja wao kumpoteza babake.Wycliff Chonge ambaye alikuwa kiongozi wa muungano wa dini katika shule hiyo alimpoteza babake Mzee Chonge akimtaja kama mtu aliyekuwa mzazi na rafiki aliyesimama naye katika kuishi kwake.

Wanafunzi wa zamani wa shule hiyo wameendelea kutuma risala za rambirambi kutoka kila pembe ya nchi.Umoja wao umetokana na vifo vilivyofuatana ikiwemo wa mkewe  phillip simiyu alifariki kutokana na ajali ya barabarani na kuzikwa kule cheranganyi na kifo cha babake peter kunania miezi michache iliyopita.

Kufikia sasa shughuli ya mipango ya mazishi inaendelea kwa kasi  huku kamati mbalimbali zikiundwa.Hizi ni baadhi rambirambi zilizotumwa....

PTER KUNANIA-May God give you strength bro,ni ngumu but take heart,pole sana,it is well my brother

PHILIP SIMIYU-Brother Wicky, Pole sana for the loss of your dearest friend, father,  and mentor may the good lord give the Chonges strength and peace at this trying moment. Rest in peace mzee.

N.K-So sorry for the loss of dad brother Wicky........may God strengthen you at this trying moments, be strong in the Lord.

JOSODOKE-Oh no! 😔 Pole Chairman.May God give you strength to bear this big loss.I have been there also and I know it's not easy😌.May God come through for you and your family

KIZITO-Pole chairman for the loss of your, May Almighty God give enough comfort at this low moments of your life

LINNET CHIRCHIR-My condolences to our brother Wycliffe chonge.May the good lord comfort your family at large in a special way

GILHAGE-Condolences to Chonge and family may the Almighty God strengthen you during this difficult period.

CHOZEN MWANGI-My condolences to chairman chonge and family

EUNICE NJERI-My condolences dear brother for this trying moment it's not easy but my almighty God comfort u n ur family


RAIS AKAIDI NA KUENDELEZA MICHANGO KANISANI HUKU AKITOA KSHS.1O MILION

 


RAIS William Ruto amefeli kudhihirisha kwa vitendo hatua yake ya kuzima maafisa wa serikali kushiriki michango ya harambee kama mojawapo ya njia za kupambana na ufisadi.

Alitoa agizo hilo Julai 2024 ili kuzima maandamano ya vijana wa Gen Z waliolalamika kuwa hulka ya viongozi na maafisa wakuu serikalini ya kutoa pesa nyingi katika michango hiyo inaendeleza uovu huo.

Wakati huo, Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, ambaye ni mwandani wa Rais Ruto, alishutumiwa kwa kutoa Sh20 milioni, wakati mmoja, katika harambee, watu wakihoji asili ya pesa hizo.

Lakini Jumapili, Septemba 15, 2024, saa chache baada ya kuwasili nchini kutoka ziara rasmi nchini Ujerumani, Dkt Ruto pamoja na wandani wake walihudhuria Ibada katika Kanisa la Stewards Revival Pentecostal, Nairobi.

Wakati wa ibada hiyo, Rais alijitolea kusaidia katika ujenzi wa jengo jipya katika kanisa hilo baada ya jengo la zamani kubomolewa kutoa nafasi kwa upanuzi wa barabara ya Outering.

Aliahidi kutoa mchango wa Sh10 milioni kufadhili mradi huo licha ya kufahamu fika kuwa wananchi wanachukia mienendo ya viongozi kutoa michango ya aina hiyo, hali iliyolazimisha serikali kuidhibiti.

“Najulikana zaidi kama mshirika mkubwa katika miradi ya ujenzi wa makanisa. Unishirikishe hapo…….. Nimekubaliana na Askofu na nitatoa Sh10 milioni kufadhili ujenzi huu,” Rais Ruto akasema waumini wa kanisa hilo wakishangilia kwa furaha.

Hata hivyo, Rais alijaribu kufafanua kwamba kile alichofanya haikuwa harambee, bali ni “mchango tu”.

“Sharti tujenge kanisa hili kwa neema ya Mungu, tatakuja hapa kuizindua,’ akasema kiongozi wa nchi.

Alipokuwa akitangaza hatua ambazo serikali yake imeweka kuzuia maafisa wakuu na watumishi wa umma kushiriki michango ya harambee, Rais Ruto aliagiza Mwanasheria Mkuu kubuni sheria ya kufanikisha hatua hiyo.

STARLINK YAIMARISHA USHINDANI


 MKURUGENZI Mkuu mteule wa Mamlaka ya Ushindani Nchini (CAK) David Kemei amewahakikishia Wakenya kwamba atazima mjadala kuhusu kampuni ya kutoa huduma za intaneti ya Sterlink baada ya Bunge kuidhinisha uteuzi wake.

Bw Kemei ambaye anatarajiwa kupigwa msasa na Kamati ya Pamoja ya Bunge la Kitaifa na Seneti kuhusu Fedha Jumanne, Septemba 17, 2024 alisema atashirikisha sekta zote katika kuleta maridhiano kati ya Starlink na kampuni zingine zinazotoa huduma hiyo nchini.

Kwenye mahojiano na Taifa Dijitali, Bw Kemei alisema anaelewa malalamishi yaliyowasilishwa dhidi ya kampuni hiyo ya Amerika na kampuni za humu nchini haswa Safaricom

“Hauwezi kutoa idhini kiholela. Sharti uangalie masuala yote, ushirikishe kampuni zote husika kabla ya kutoa mwelekeo utakaowafaa wadau hao wote,” Bw Kemei akasema.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo mteule alizitaka kampuni za humu nchini na wadau wengine katika sekta ya mawasiliano kukumbatia teknolojia bora ili kuimarisha huduma kwa Wakenya.

“Uzuri wa ujio wa Starlink ni kwamba utazilazimu kampuni za hudumu nchini kuwa wabunifu na kukumbatia mbinu za kisasa katika utoaji huduma. Tunataka kampuni za hapa nchini zitikiswe ili zitupe huduma bora, ndipo kusema ni kampuni inayotangaza faida ya mabilioni ya fedha ilhali maeneo mengine ya nchi hayajaunganishwa na intaneti,” Bw Kemei akasema

Alisema kuwa atahakikisha kuwa wadau wote wameshirikishwa katika kupatikana kwa mwafaka kuhusu suala hilo kuhakikisha kuwa kila mtu anapata nafasi ya kuhudumu huku kampuni za humu nchini zikilindwa dhidi ya ushindani usiofaa.

Kulingana na Bw Kemei, baadhi ya kampuni za humu nchini zimewekeza mabilioni ya fedha katika miundomsingi, rasilimali ambazo haziwezi kuruhusiwa zifutiliwe na ujio wa kampuni mpya ya kutoa huduma za intaneti.

Alisema masuala kama vile usalama wa nchini na ulinzi wa data yanapaswa kuzingatiwa kabla ya kuidhinisha Starlink kutoa huduma za intaneti kwa Wakenya.

Sunday, 15 September 2024

WAKENYA WAONGEZEKA JELA ZA MAREKANI

 


UFICHUZI wa hivi majuzi wa kukamatwa na kufungwa kwa aliyekuwa mgombea urais Mohamed Abduba Dida unaongeza orodha ya raia wa Kenya wanaotumikia kifungo jela nchini Amerika.

Mwalimu huyo wa zamani ambaye aliwania urais mwaka wa 2013 na 2017 kwa sasa anazuiliwa katika gereza la Big Muddy huko Illinois baada ya kupatikana na hatia ya kumnyemelea na kumtisha mkewe waliyetengana.

Wakenya wengine mashuhuri waliozuiliwa nchini Amerika ni wana wawili wa Akasha waliopatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya na pia kuzuia haki kwa kutoa hongo kwa maafisa wa Kenya katika jitihada za kuepuka kupelekwa Amerika kushtakiwa.

Baktash Akasha alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela mwaka wa 2019 huku Ibrahim Akasha akihukumiwa miaka 23 mnamo 2020.

Ndugu hao wa Akasha walikamatwa Mombasa mnamo Novemba 2014 katika oparesheni iliyoongozwa na Amerika.

Huenda kifungo kirefu zaidi ni cha Brian Musomba Maweu aliyehukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 2015 kwa kuhusika na ponografia ya watoto.

Mwaka wa 2014, alichapisha jumbe 121 kwenye tovuti ya Dreamboard–mtandao wa kibinafsi wa wanachama pekee ambao ulikuza unyanyasaji wa kingono na unyanyasaji wa watoto wadogo.

Kevin Kang’ethe ambaye aligonga vichwa vya habari baada ya kutoroka kituo cha polisi pia sasa anazuiliwa gerezani nchini Amerika baada ya kurejeshwa humo wiki mbili zilizopita.

Anakabiliwa na kesi ya mauaji ya kinyama ya mpenzi wake Margaret Mbitu mwaka jana, 2024. Alitoroka Amerika hadi Kenya baada ya kufanya uhalifu huo lakini maafisa walifuatilia na kumkamata.

Akiwa kizuizini katika kituo cha polisi cha Muthaiga, alitoroka katika hali isiyoeleweka na alikamatwa tena na kurudishwa Amerika kwa ndege ya kibinafsi ya FBI kujibu mashtaka ya mauaji.

Mnamo Septemba 3, 2024 alikana mashtaka na amepangwa kurejea kortini Novemba 5 kesi kusikilizwa. Anazuiliwa bila dhamana.

Ulaghai ukiwemo ulaghai wa mapenzi na ulaghai wa uwekezaji ni baadhi ya uhalifu ambao umepelekea baadhi ya Wakenya kufungwa gerezani Amerika siku za hivi majuzi.

Mnamo Februari Paul Maucha, 59, alipatikana na hatia ya njama ya kuwalaghai watu kwa kuwahadaa walipe pesa kwa kampuni kwa kisingizio kwamba wangepokea faida nzuri za kifedha baadaye.

Mwaka jana, 2023, Florence Mwende Musau alifungwa jela kwa kushiriki katika njama iliyohusisha ulaghai wa mapenzi iliyobuniwa kuwahadaa waathiriwa kutuma pesa kwa akaunti za benki zilizodhibitiwa naye na watu wengine.

Alipatikana na hatia ya kutumia pasipoti ghushi zenye majina tofauti kufungua akaunti za benki ambapo angepokea pesa kutoka kashfa za mapenzi.


Mnamo Mei 2023, mahakama ilimhukumu Abdi Hussein Ahmed kifungo cha miaka minne kwa kula njama ya kusafirisha kiasi kikubwa cha pembe za kifaru na pembe za ndovu za thamani ya mamilioni ya pesa.

Pia, alipatikana na hatia ya kulangua heroin.

Mnamo Januari, Erick Gachuhi Wanjiku, 42, alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuwashambulia maafisa wa serikali.

MOTO WATEKETEZA SHULE MACHAKOS JUMAPILI

MKASA wa moto umeripotiwa katika Shule ya Upili ya Katoloni iliyoko Kaunti ya Machakos. Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu Nchini (KRC), moto huo ulitokea dakika chache baada ya saa tatu za usiku wa Jumamosi, Septemba 14, 2024. “Kisa cha moto kimeripotiwa katika Shule ya Upili ya Katoloni iliyoko Kaunti ya Machakos. Juhudi za kuuzima zinaendelea,” KRC ikasema kwenye ujumbe kupitia akaunti yake ya X. Hata hivyo, baadaye wafanyakazi wa shirika hilo la kushughulikia majanga wakishirikiana na wale wa Idara ya Zimamoto katika serikali ya Kaunti ya Machakos walifaulu kudhibiti na kuzima moto huo. “Shirika la Msalaba Mwekundu pia linatoa huduma ya kwanza katika eneo la tukio,” KRC iliandika kwenye X, baada ya muda wa saa tatu. Duru zinasema kuwa wanafunzi wawili walikimbizwa katika Hospitali ya Machakos Level 5, baada ya kuathiriwa na moshi uliotokana na moto huo. Visa kadhaa vya moto kuteketeza mali vimeripotiwa katika shule kadha nchini mwezi huu wa Septemba. Mkasa mbaya zaidi ulikuwa ni ule uliotokea usiku wa kuamkia Ijumaa, Septemba 6, 2024 Hillside Endarasha Academy, Nyeri ambapo jumla ya wanafunzi 17 walikufa papo hapo. Wengine wanne walikufa hospitalini kutokana na majeraha ya moto na hivyo kufikisha idadi jumla ya waliokufa kuwa 21.

Saturday, 14 September 2024

GEN Z WAAPA KUSIMAMA NA GACHAGUA

 


VIONGOZI wa vijana kutoka Mlima Kenya wamewashutumu Wabunge  ambao wamejitenga na Naibu Rais Rigathi Gachagua na kumwidhinisha Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Msemaji wa eneo hilo.

Wakiongozwa na Mtaalamu wa Usawa wa Jinsia, Dkt Fridah Karani, viongozi hao walishutumu wabunge hao kwa kujihusisha na siasa za migawanyiko badala ya kuangazia maendeleo ya eneo hilo.

Walijitenga na wabunge hao, wakisema hawakushauriwa.’Hakukuwa na ushiriki wa umma na kwa hivyo tunakataa uamuzi wa wabunge,’ alisema Dkt Karani.

Vijana waliapa kupinga hatua yoyote ya kugawanya eneo hilo.’Sisi kama vijana, hatuwezi kusimama na kutazama jinsi siasa za migawanyiko na ajenda za ubinafsi zinatishia umoja wetu, utulivu na maendeleo,’ alisema.

Vijana walisisitiza kuwa ajenda ya mgawanyiko inayoenezwa na wabunge inaonyesha kutojali kabisa usawa wa kijinsia na maendeleo ya eneo lao.

‘Vijana na wanawake wanatengwa katika mijadala muhimu ya kisiasa licha ya kikatiba kuamuru kujumuishwa kwao,’ alisema Dkt Karani.Wabunge 14 kutoka kaunti za Embu, Meru na Tharaka Nithi walitangaza kwamba Prof Kindiki atakuwa msemaji wao wa kuuunganisha eneo hilo na serikali ya Rais William Ruto.

Mnamo Alhamisi, wabunge 48 wa eneo la Mlima Kenya Magharibi pia walijitenga na Bw Gachagua na kumuunga Profesa Kindiki kuwa msemaji wao.

Wabunge walisema wameungana kushawishi maendeleo ya Mlima Kenya.

“Kama viongozi waliochaguliwa kutoka Mlima Kenya, kwa niaba yetu na wakazi waliotuchagua, tumeamua kuwa atakayetuunganisha na serikali kuu ni Profesa Kindiki,” walisema katika taarifa.

Wabunge hao wanaotoka kaunti za Kiambu, Murang’a, Nyeri, Nyandarua, Kirinyaga, Nakuru, Laikipia na Nairobi, walisema<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5352755744671694"

     crossorigin="anonymous"></script> Bw Gachagua ameshindwa kuonyesha uongozi bora na kukataa kuungana na Rais kuwaunganisha Wakenya.

“Juhudi zetu za kusaka maendeleo kwa watu wetu zimetatizwa na kukosekana kwa kiongozi ambaye anatuelewa na anayeweza kupeleka maslahi ya watu wetu kwa serikali kuu.

“Hata hivyo, Seneta wa Kirinyaga Kamau Murango na Mwakilishi wa Wanawake Njeri Maina wamejitenga na wabunge hao wakisema hawakuhusisha maoni ya wakazi wa eneo hilo. Walisisitiza kuwa wabunge hao wamepoteza mwelekeo wa kisiasa, wakionya kuwa huenda wakapoteza viti vyao katika uchaguzi ujao. Wabunge hawa wamekosea na wakazi kutoka eneo hili hawajafurahishwa nao,’ alisema Bw Murango.

Bi Maina alitaja hatua ya wabunge hao kama aibu kwa eneo lao.

‘Naibu Rais ndiye mwanasiasa mkuu kutoka eneo letu lakini cha kusikitisha ni kwamba wabunge wanapigana naye,’ alisema.

Bi Njeri aliapa kuendelea kumuunga mkono Bw Gachagua ambaye alisema ana nia nzuri kwa eneo la Mlima Kenya.

‘Adui zangu wa kisiasa wananiita mfuasi shupavu wa Bw Gachagua. Ni kweli na nitaendelea kumuunga mkono kwa sababu ni kiongozi mzalendo wa Milimani,’ alisema Bi Njeri.


MTOTO ATOBOA KUWA BABAKE AMEFARIKI KISUMU HUKU BIW SAMINZI LIKITANDA

 

KIINI cha mwanaume mwenye umri wa miaka 39 kujiua akiwa nyumbani mwake Manyatta viungani mwa jiji la Kisumu kingali kitendawili kwa jamaa na majirani.

Kinachojulikana kufikia sasa ni kuwa Washington Obat aligombana na mkewe Caroline Achieng mara kadhaa Alhamisi kabla ya tukio hili la kutatanisha kusababisha wingu la simanzi kutanda eneo la Manyatta.

Mke wa marehemu anasimulia kuwa walikuwa na mzozo Alhamisi jioni.

Baada ya mzozo, mume wake alimwomba msamaha warudieni na kuendeleza familia.

Ilikuwaje baadaye Obat ‘alijitia kitanzi’?

Mzozo mkali

Mkazi huyu wa Wadi ya Kondele anafichua kuwa walikabiliana vikali na mumewe katika patashika iliyomsabibishia majeraha mwilini.

Kulingana na Achieng’, isingalikuwa shangazi za mume wake, pia yeye angekuwa marehemu kama mume wake.<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5352755744671694"

     crossorigin="anonymous"></script>

“Kwa bahati nzuri niliokolewa na shangazi zake na ilibidi nilale kwa majirani kuepuka hatari zaidi,” alisimulia.

“Alikuja kwa familia yangu na kunishawishi kwamba turudi nyumbani na tukapatana. Baadaye aliondoka kuelekea kazini lakini alirudi akiwa mlevi na kuanza kunisumbua huku akiniuliza nina tatizo gani. Hapo ndipo alifunga mlango na kuanza kunipiga. Nilijaribu kutoroka na kuripoti katika kituo cha polisi cha Manyatta.”

Achieng anaeleza kwamba alimtuma mwanawe nyumbani kwao kuchukua sare za shule.

Kwa bahati mbaya, anasema, mtoto wake alikutana na mwili wa baba ukilala bila pumzi.

“Nilikuwa nimemtuma mwanangu aende kuchukua sare yake kutoka nyumbani Ijumaa asubuhi lakini alimkuta baba yake tayari amekufa,” alisema.

Chifu Msaidizi wa Kata ndogo yaa Manyatta A, Agnes Akinyi alithibitisha kisa hicho na kufichua kuwa ripoti hiyo ilitumwa kituoni na mzee wa kijiji cha eneo hilo Isaac Opiyo.

“Tulipokea ripoti kutoka kwa mzee wa kijiji chetu Opiyo, kwamba mwanamume anayejulikana kama Washington Obat amejiua kufuatia ugomvi wa kifamilia,” Akinyi alifichua.

Chifu huyo msaidizi alitoa wito kwa wanandoa kutafuta usaidizi kutoka kwa afisi za serikali na mashirika mengine ya eneo hilo wakati wowote ndoa zao zinaingia doa.

Aliwaonya wanandoa dhidi ya kujichukulia sharia mkononi.

“Ikiwa wanandoa wanatofautiana basi ni bora kutafuta suluhu ya amani badala ya kujitoa uhai kwa sababu hiyo si suluhu,” alitanguliza. “Ombi langu kwa wanandoa ni kuwa karibu na afisi za serikali ili kusaidia kutatua masuala yao,”

Kadhalika, Bi Akinyi aliwahimiza wakaazi kutambua dalili za mizozo inayoweza kuwaletea balaa baadaye.

Wanapotambua changamoto za awali, aliendelea, wanafaa kushirikiana na kuhusisha uongozi wa mtaa kuwasaidia.

Monday, 9 September 2024

MKUU WA BARAZA LA MAWAZIRI MSALI MUDAVADI AELEKEA NAMIBIA KUMPIGIA DEBE RAILA- AUC


 MKUU wa Mawaziri na Waziri wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi anaelekea Namibia ambako anatarajiwa kumpigia debe Raila Odinga katika azma yake ya kutaka achaguliwe mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

Bw Mudavadi, ambaye aliondoka Jumapili pia ameratibiwa kufanya mashauriano na viongozi wakuu wa Namibia akilenga kuimarisha mahusiano kati ya Kenya na nchi hiyo katika nyanja kadhaa za kimaendeleo.

Hata hivyo, afisi yake ilisema kwenye taarifa kwamba ajenda kuu ya ziara yake ni kumpigia debe Bw Odinga atakapokutana Makamu wa Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah.

“Mudavadi atatumia nafasi hiyo kuvumisha azma ya Raila Odinga katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) mnamo Februari 2025,” ikasema taarifa iliyotumwa kwa vyombo na Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari katika afisi ya Mudavadi Jacob Ng’etich.

Ziara hii ni ya kwamba ya kusaka uungwaji mkono kwa Bw Odinga katika eneo la Afrika Kusini baada ya kuzinduliwa kwake jijini Nairobi.

Hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya Nairobi ilihudhuriwa na baadhi ya marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kenya imewasilisha mwaniaji wa uenyekiti wa AUC kwa mara ya pili mfufulizo baada ya aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Kigeni Amina Mohamed kushindwa na mwenyekiti anayeondoa Moussa Faki Mahamat mnamo 2017.

Bw Odinga anashindana na wagombeaji wengine watatu ambao ni Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Djibouti Mohamoud Ali Youssouf, aliyekuwa waziri wa masuala ya kigeni wa Mauritius Anil Kumarsigh Gayan na Waziri wa zamani wa Masuala ya Kigeni wa Madagascar Richard Randriamandrato.

Hata hivyo, inabashiriwa kuwa Youssouf ambaye amehudumu kama Waziri wa Masuala ya Kigeni kwa miaka 10 ndiye mshindani mkuu wa Bw Odinga.

Ziara ya Mudavadi nchini Namibia inajiri baada ya Bw Odinga kuungana na ujumbe wa Rais William Ruto katika mkutano wa mashauriano kati ya marais wa Afrika na China kuhusu masuala ya maendeleo (FOCAC) wiki jana jijini Beijing, China.

Wakati wa mkutano huo, Rais Ruto alifanya mikutano tofauti na marais sita wa Afrika kumpigia debe Bw Odinga.

Kando na kumfanyia kampeni Bw Odinga, Bw Mudavadi anatarajiwa kutetea kuimarishwa kwa mahusiano kati ya Kenya na Namibia na kuanzisha kwa ubalozi wa Kenya jijini Nairobi.

Aidha, atatetea kuimarishwa kwa biashara kati ya Kenya na Namibia kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Kulingana na ripoti kutoka kwa Wizara za Masuala ya Kigeni na Biashara nchini Kenya imekuwa ikiagiza bidhaa za thamani ya Sh117.76 milioni kutoka Namibia na kuuza bidhaa za thamani ya Sh106.31 milioni nchini Namibia ndani ya kipindi cha mwongo mmoja.

Imetafsiriwa na Charles Wasonga 

KENYA:DCI YAANZISHA UCHUNGUZI KUHUSU MKASA WA MOTO ULIOTEKETEZA WANAFUZI 21 HADI KIFO


 MAAFISA wa upelelezi wanakusanya maelezo yanayotarajiwa kusaidia kutegua kitendawili kuhusu chanzo cha moto kilichosababisha vifo vya wanafunzi 21 katika Shule ya Hillside Endarasha Academy, Kieni, Nyeri.

Miili ilipelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Naromoru Level Four kufanyiwa ukaguzi na vipimo vya chembechembe za DNA kuitambua.

Mwanapatholojia wa serikali Dkt Johansen Oduor, Jumapili alisema vipimo vya DNA vitaanza kufanywa, Jumatatu, Septemba 9, 2024.

Jumapili, wahudumu katika hifadhi hiyo ya maiti walikuwa wakiandaa miili hiyo kabla ya wanapatholojia kuwasili.

Hifadhi hiyo inaendelea kujengwa na haijakamilika.

Maswali

Maswali yameulizwa kuhusu chanzo cha moto huo japo madai yameibuliwa kuwa huenda ulisababishwa na kulipuka kwa balbu ya stima.

Hata hivyo kuna wazazi ambao wamepinga nadharia hiyo, wakidai Alhamisi wanafunzi walidaiwa kuibua malalamishi kuhusu masuala fulani shuleni humo.

Mzazi aliyeongea na Taifa Leo Dijitali, na akaomba tulibane jina lake, alisema alipata habari hizo kutoka kwa mwanawe ambaye ni mwanafunzi wa kutwa.

Alisema mvulana huyo  wa Gredi 7, alimweleza kuwa mwendo wa saa kumi za jioni baadhi ya wanafunzi walikaa “kwa muda mrefu” katika bweni lililoteketea “wakijadili masuala fulani” ambayo sio ya kawaida.

Usimamizi wa shule hiyo haujatoa taarifa zozote tangu kutokea kwa mkasa huo.

“Baadhi ya wanafunzi walikaa kwa muda mrefu katika bweni na mwanangu aliniambia kulikuwa na wasiwasi shuleni kuhusu mambo yasiyojulikana.

Watoto huwa hawaruhusiwi kwenda katika bweni nyakati za mchana. Wakitaka kwenda huko, sharti waandamane na msimamizi wa mabweni wachukue kile wanachotaka kisha warejee madarasani mara moja. Mbona kanuni hii haikuzingatiwa?”, akauliza.Mzazi huyo pia alisema kuwa mwendo wa saa  nne usiku, kuna mwanafunzi aliyempigia simu mzazi wake na kupasha habari kuhusu kutokea kwa moto.

“Swali ni je, simu hiyo ilikuwa ya nani na ni mzazi yupi huyu alipigiwa simu?” mzazi huo akauliza.

“Tunafahamu fika kwamba watoto hawaruhusiwi kutumia simu za mkono wakiwa shule na hufanya hivyo tu baada ya kupata kibali maalum na chini ya usimamizi wa mwalimu mhusika. Tunataka mzazi huyu aliyepigiwa simu ajitokeze na kutoa maelezi kwa maafisa wa upelelezi ili ibainike kilichotendeka.” Mzazi huyo akasema.

Maafisa hao wa upelelezi wa vifo, wakiongozwa na Martin Nyuguto, waliendelea kusaka ushahidi katika eneo la mkasa huku serikali ikisema watoto 48 bado hawajulikani waliko kufikia Jumapili, Septemba 8, 2024 jioni.

Lakini Ijumaa Septemba 6, 2024, Naibu Rais Rigathi Gachagua alisema watoto 70 hawakujulikana waliko.

Alibashiri kuwa walipewa hifadhi katika makazi  ya karibu na Shule ya Hillside Endarasha Academy, walikokimbilia moto ulipotokea.

Jumapili, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki jimbo la Nyeri, Anthony Muheria, alitoa wito kwa wazazi waliwachukua watoto baada ya mkasa kupiga ripoti kwa maafisa wa usalama ili kuzima dukuduku kuhusu idadi ya watu ambao hawajulikani waliko.

“Ikiwa mtoto wako yuko nyumbani wapashe maafisa wa upelelezi ili wajue kwamba wako salama. Watoto hao pia wanafaa kupewa ushauri nasaha kutokana na mshtuko uliowapata wakati wa mkasa huo wa moto,” Askofu Muheria akasema wakati wa ibada ya pamoja na kuombea waliofuka na kuzifariji jamaa zilizopoteza watoto wao.

MAANDAMANO YA WANAFUNZI KENYA

Mmoja wa wanafunzi wa somo la udaktari katika Chuo Kikuu cha Moi waliandamana mjini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, kupinga mfumo mpya wa ufadhili wa elimu ya chuo kikuu mnamo Septemba 9, 2024. PICHA | JARED NYATAYA

 WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Moi bewa kuu la  Kesses mjini Eldoret waliandamana Jumatatu wakitaka kufutiliwa mbali au kubadilishwa kwa mfumo mpya wa ufadhili wa masomo ya chuo kikuu.

Yalijiri licha ya viongozi wa kitaifa wa wanafunzi wa vyuo vikuu kupiga breki maandamano waliyopanga kufanya kote nchini kuanzia wiki hii, baada ya serikali kuahidi kwamba ungetathmini upya mfumo huo wa kufadhili elimu ya juu.

Hata hivyo, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Moi walishiriki maandamano kwa kuimba nyimbo za kupinga serikali na kubeba mabango yaliyopinga mtindo huo mpya wa ufadhili. Waliwataja viongozi wao wa kitaifa kama wasaliti.

 “Kama Chuo Kikuu cha Moi tunashikilia msimamo wetu kwamba tunakataa mtindo huu wa ufadhili. Siku 30 ambazo serikali imeomba ili kutathmini upya mfumo huo ni njama ya kutufumba macho hadi mwisho wa muhula wa sasa wa masomo,” alisema Enock Kwena mmoja  wa viongozi wa wanafunzi katika chuo hicho.

Wanafunzi hao walishutumu serikali kwa kutojali masaibu ya wanachuo.

Walisema hawana imani kamwe na utawala wa sasa na hususan ahadi iliyotolewa na Waziri wa Elimu Julius Ogamba; ya kuundwa kwa kamati mbili zitakazotathmini mfumo huo mpya wa ufadhili, akitoa wito kwa wanafunzi kuwa watulivu.

“Ahadi zilizotolewa na serikali ni mbinu za kudumisha mfumo huu haramu ilhali tunaendelea kuteseka. Mfumo huo utaishia kuleta ubaguzi wa kielimu nchini badala ya usawa,” mwanafunzi mwingine wa chuo cha Moi alisema wakati wa maandamano hayo katika lango<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5352755744671694"

     crossorigin="anonymous"></script>