HABARI KUU:

GACHAGUA ALIYEMUITA RAILA MAJINA SASA AMMEZEA MATE 2027..//..LUSAKA AMKAUKIA SENETA ONYONKA KWA KUMUITA MPUMBAVU!..//..GEN Z WA BANGALADESH WAVAMIA IKULU YA WAZIRI MKUU..//..AJALI SACHANGWAN HUKU WANAFUNZI 25 NA WAALIMU 3 WAKIPATA MAJERAHA MABAYA..//..MGOMBEA urais wa Chama cha Democrat Kamala Harris amemteua Gavana wa Minnesota Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa urais wa Novemba 5, mwaka huu.// AMERIKA imeonya serikali ya Kenya Kwanza dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi kukabili waandamanaji na kutaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu..//GAVANA wa Meru Kawira Mwangaza anataka Mahakama Kuu kuwahukumu maafisa wawili wa bunge la kaunti na MCA aliyeteuliwa kwa madai walidharau mahakama, akisema walipuuza maagizo ya korti kwa kukusudia kumtimua kwa mara ya tano.

Monday, 9 September 2024

MAANDAMANO YA WANAFUNZI KENYA

Mmoja wa wanafunzi wa somo la udaktari katika Chuo Kikuu cha Moi waliandamana mjini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, kupinga mfumo mpya wa ufadhili wa elimu ya chuo kikuu mnamo Septemba 9, 2024. PICHA | JARED NYATAYA

 WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Moi bewa kuu la  Kesses mjini Eldoret waliandamana Jumatatu wakitaka kufutiliwa mbali au kubadilishwa kwa mfumo mpya wa ufadhili wa masomo ya chuo kikuu.

Yalijiri licha ya viongozi wa kitaifa wa wanafunzi wa vyuo vikuu kupiga breki maandamano waliyopanga kufanya kote nchini kuanzia wiki hii, baada ya serikali kuahidi kwamba ungetathmini upya mfumo huo wa kufadhili elimu ya juu.

Hata hivyo, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Moi walishiriki maandamano kwa kuimba nyimbo za kupinga serikali na kubeba mabango yaliyopinga mtindo huo mpya wa ufadhili. Waliwataja viongozi wao wa kitaifa kama wasaliti.

 “Kama Chuo Kikuu cha Moi tunashikilia msimamo wetu kwamba tunakataa mtindo huu wa ufadhili. Siku 30 ambazo serikali imeomba ili kutathmini upya mfumo huo ni njama ya kutufumba macho hadi mwisho wa muhula wa sasa wa masomo,” alisema Enock Kwena mmoja  wa viongozi wa wanafunzi katika chuo hicho.

Wanafunzi hao walishutumu serikali kwa kutojali masaibu ya wanachuo.

Walisema hawana imani kamwe na utawala wa sasa na hususan ahadi iliyotolewa na Waziri wa Elimu Julius Ogamba; ya kuundwa kwa kamati mbili zitakazotathmini mfumo huo mpya wa ufadhili, akitoa wito kwa wanafunzi kuwa watulivu.

“Ahadi zilizotolewa na serikali ni mbinu za kudumisha mfumo huu haramu ilhali tunaendelea kuteseka. Mfumo huo utaishia kuleta ubaguzi wa kielimu nchini badala ya usawa,” mwanafunzi mwingine wa chuo cha Moi alisema wakati wa maandamano hayo katika lango<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5352755744671694"

     crossorigin="anonymous"></script>

No comments:

Post a Comment