HABARI KUU:

GACHAGUA ALIYEMUITA RAILA MAJINA SASA AMMEZEA MATE 2027..//..LUSAKA AMKAUKIA SENETA ONYONKA KWA KUMUITA MPUMBAVU!..//..GEN Z WA BANGALADESH WAVAMIA IKULU YA WAZIRI MKUU..//..AJALI SACHANGWAN HUKU WANAFUNZI 25 NA WAALIMU 3 WAKIPATA MAJERAHA MABAYA..//..MGOMBEA urais wa Chama cha Democrat Kamala Harris amemteua Gavana wa Minnesota Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa urais wa Novemba 5, mwaka huu.// AMERIKA imeonya serikali ya Kenya Kwanza dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi kukabili waandamanaji na kutaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu..//GAVANA wa Meru Kawira Mwangaza anataka Mahakama Kuu kuwahukumu maafisa wawili wa bunge la kaunti na MCA aliyeteuliwa kwa madai walidharau mahakama, akisema walipuuza maagizo ya korti kwa kukusudia kumtimua kwa mara ya tano.

Monday, 5 January 2026

AJALI MBAYA KUMI WAKIAGA

 WATU 10 wamethibitishwa kufa baada ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Jumatatu katika eneo la Karai, kwenye barabara kuu ya Nairobi–Nakuru karibu na mji wa Naivasha.<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5352755744671694"

     crossorigin="anonymous"></script>

Polisi na wahudumu wa dharura walisema ajali ilitokea karibu saa tano usiku, wakati basi la abiria lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Magharibi ilipogongana na matatu.

Kwa mujibu wa maafisa, watu wanane waliangamia papo hapo, wakijumuisha abiria wa matatu.

Idadi ya waliofariki iliongezeka hadi 10 baada ya majeruhi wawili kufariki wakitibiwa katika Hospitali ya Kaunti ya Naivasha, ambapo takriban watu 35, wakiwemo watoto watano, walihudumiwa.

Maafisa wa polisi walisema uchunguzi unaendelea ili kubaini sababu kamili ya ajali huku ikisemekana basi lilikuwa likijaribu kupita magari wakati wa msongamano.

Ajali hiyo inajiri siku chache baada ya ajali nyingine ya barabarani kuripotiwa katika eneo hilo iliyomuua aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo.<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-5352755744671694"

     crossorigin="anonymous"></script>

No comments:

Post a Comment