Mzee Emilio Mwai Kibaki alizaliwa tarehe 15
mwezi Novemba mwaka 1931, katika kijiji cha Gatuyaini Kaunti ya Nyeri. Rais wa
tatu Mwai Kibaki akiwa kwenye hafla iliyopita.
Wazazi wa Kibaki wakiwa marehemu Kibaki
Githinji na marehemu Teresia Wanjiku, na alikuwa kitinda mimba katika familia
ya watoto wanane. Kibaki alibatizwa Emilio Stanley na wamishenari wa
ki-Italiano akiwa kijana, lakini amekuwa akitumia jina Mwai Kibaki katika
maisha yake. Historia Kuhusu Elimu ya Mwai Kibaki Kibaki alianza elimu yake
katika shule ya msingi ya Gatuyainĩ, kisha akajiunga na shule mishenari ya
Karima na baadaye kujiunga na shule ya upili ya Mathari ambayo kwa sasa
inajulikana kama Nyeri High.
Nyakati za likizo za shule, Kibaki alikuwa manamba katika mabasi yaliyojulikana kama Othaya African Bus Union. Hayati Kibaki alijiunga na shule ya upili ya Mang’u mwaka wa 1947 hadi 1950. Alipita vizuri sana kwa kupata alama sita na hivyo kumsababisha kujiunga na chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, alikosomea historia na sayansi kuhusu siasa. Baada ya kukamilisha elimu ya chuo kikuu, Kibaki aliajiriwa na kampuni ya kuuza mafuta ya Shell tawi la Uganda akiwa meneja wa mauzo. Baadaye Kibaki alijiunga chuo kikuu cha Uingereza kuhusu uchumi, alikosomea usimamizi wa fedha za umma. Mnamo mwaka 1958, kibaki alirejea katika chuo kikuu cha Makerere ambapo alikuwa naibu wa mhadhiri katika kitengo cha uchumi wadhifa alioushikilia hadi mwaka 1961. Mwaka 1961,
Kibaki alifunga pingu za maisha na Lucy
Muthoni. Kazi alizofanya Mwai Kibaki Licha ya kuwa mbunge wa Othaya, Kibaki
amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa
Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya
kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Kibaki
Kibaki Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mvutano na Rais msaafu Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya. Mwaka 1991 Kibaki aligura chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 akaibuka wa pili. Kibaki aliingia mamlakani mwaka wa 2002, na kufaulu kumrithi Hayati Daniel Arap Moi aliyekuwa madarakani kwa miaka 24. Uchaguzi wa 28 Disemba 2007 ulimrejesha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani, ODM na kusababisha kuundwa kwa serikali ya nusu mkate. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment