Friday 22 April 2022

MWANAMUZIKI EDNA NABWIRE KUTOKA JIMBO LA BUNGOMA

  • Mwanamuziki anayeibukia bi.Edna Nabwire 
  • atakuwa anazindua album yake ya kwanza hivi karibuni.Edna ambaye ni mshirika wa dhehebu la Jesus Adoration Family yupo kwenye mikakati ya uzinduzi wa album hii yenye nyimbo tano.Anaelezea pakubwa kuhusu magumu ya maisha mbayo hayafai kukuvunja moyo ama kusababisha uchoke na maisha.Anaelezea kukataliwa na wanadamua laiyesimama nao wakati wa ugumu wao lakini walimgeuka.


 

PICHA ZA RAIS KIBAKI UJANA NA UZEE HADI KIFO CHAKE.





 

HISTORIA FUPI YA HAYATI MZEE MWAI KIBAKI [ 1931-2022]

 


Mzee Emilio Mwai Kibaki alizaliwa tarehe 15 mwezi Novemba mwaka 1931, katika kijiji cha Gatuyaini Kaunti ya Nyeri. Rais wa tatu Mwai Kibaki akiwa kwenye hafla iliyopita.

Wazazi wa Kibaki wakiwa marehemu Kibaki Githinji na marehemu Teresia Wanjiku, na alikuwa kitinda mimba katika familia ya watoto wanane. Kibaki alibatizwa Emilio Stanley na wamishenari wa ki-Italiano akiwa kijana, lakini amekuwa akitumia jina Mwai Kibaki katika maisha yake. Historia Kuhusu Elimu ya Mwai Kibaki Kibaki alianza elimu yake katika shule ya msingi ya Gatuyainĩ, kisha akajiunga na shule mishenari ya Karima na baadaye kujiunga na shule ya upili ya Mathari ambayo kwa sasa inajulikana kama Nyeri High.

Hayati kibaki na hayati moi
Nyakati za likizo za shule, Kibaki alikuwa manamba katika mabasi yaliyojulikana kama Othaya African Bus Union. Hayati Kibaki alijiunga na shule ya upili ya Mang’u mwaka wa 1947 hadi 1950. Alipita vizuri sana kwa kupata alama sita na hivyo kumsababisha kujiunga na chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, alikosomea historia na sayansi kuhusu siasa. Baada ya kukamilisha elimu ya chuo kikuu, Kibaki aliajiriwa na kampuni ya kuuza mafuta ya Shell tawi la Uganda akiwa meneja wa mauzo. Baadaye Kibaki alijiunga chuo kikuu cha Uingereza kuhusu  uchumi, alikosomea usimamizi wa fedha za umma. Mnamo mwaka 1958, kibaki alirejea katika chuo kikuu cha Makerere ambapo alikuwa naibu wa mhadhiri katika kitengo cha uchumi wadhifa alioushikilia hadi mwaka 1961. Mwaka 1961,

Kibaki alifunga pingu za maisha na Lucy Muthoni. Kazi alizofanya Mwai Kibaki Licha ya kuwa mbunge wa Othaya, Kibaki amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Kibaki

Kibaki Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mvutano na Rais msaafu Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya. Mwaka 1991 Kibaki aligura chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 akaibuka wa pili. Kibaki aliingia mamlakani mwaka wa 2002, na kufaulu kumrithi Hayati Daniel Arap Moi aliyekuwa madarakani kwa miaka 24. Uchaguzi wa 28 Disemba 2007 ulimrejesha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani, ODM na kusababisha kuundwa kwa serikali ya nusu mkate. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.